Wednesday, 29 November 2017

CCM YASHINDA KATA 42 KATI YA 43 ZA UDIWANI NCHINI NZIMA

Mikoani. Matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 uliofanyika jana Jumapili yameonyesha kuwa CCM imevigaragaza vyama vya upinzani katika kata mbalimbali baada ya wagombea wake kushinda.

Katika Kata ya Mamba wilayani Lushoto mkoani Tanga, Richard Msumari(CCM) alishinda kwa kura 1,399 akiwashinda Jafari Ndege(Chadema) kura 774 na Nurdini Kipingu(CUF) kura 30.

Kwenye kata hiyo jumla ya kura zilizopigwa ni 958 zilizoharibika ni 3 halali ni 955.

Katika Kata ya Majengo wilayani Korogwe mkoani Tanga, Mustapha Shengwatu (CCM) alishinda kwa kura 527 na kuwashinda Abdallah Maonga(Chadema) aliyepata kura 385, Abbas Chomboko (ADC ) kura 17 na Kassim Msenga (CUF) kura 26.

Katika Kata ya Bomambuzi mkoani Kilimanjaro, Juma Raibu (CCM) alishinda kwa kura 2,854, Hedlack Minde (Chadema) 1,992, Salim, Mchomvu ( CUF) 17, Issack Kireti( Sau) 00 na Reuben Msuya (UDP) 02

Machame Magharibi: Martin Munisi(CCM) kura 1,048 na Bariki Lema(Chadema) 595,

Mnadani: Nasibu Mndeme(CCM) 1,708, Ezra Nyari( Chadema) 958, Msafiri Hamisi (ACT-Wazalendo) 14 na Maynard Shoo(NCCR-Mageuzi) 3.

Weruweru: Swalehe Msengesi (CCM)1,410, Moses Kalaghe (Chadema) 706, Haji Ndarai (CUF) 26, Mabranda Msabaha(ACT-Wazalendo) 3 na Friman Massawe (NCCR-Mageuzi) 00.

Katika Mkoa wa Arusha CCM imeshinda kata zote tano baada ya Chadema kujitoa na matokeo ni kama ifuatavyo.

Kata ya Makiba, Samson Laizer(CCM) 2,029, Joyce Martin(Chadema) 608. Kata ya Ambuleni, Jasephat Jackson(CCM) 2,057 na Dominick Mollel(Chadema) 1,201.

Kata ya Leguruki, Andason Sikawa(CCM) 3,023 na Daniel Mbise(Chadema) 287.

Kata Maroroni, Yoha Kaaya(CCM) 3,568 na Asanterabi Mbise(Chadema) 1,201.

Kata Ngabobo, Solomon Laizer(CCM) 820 na Emmanuel Salewa(Chadema) 353.

Kata ya Moita Monduli, Prosper Damuni (CCM) 1,563, Lobulu Kivuyo (Chadema) 1,419, Mungey Laizer (ACT) 10 na Henry Machota (NRA) 0.

Katika Mkoa wa Mbeya matokeo ya jumla Kata ya Ibighi_Rungwe, mgombea Chadema, Lusubilo Simba alipata kura 1,449 akifuatiwa na Suma Fyandomo wa CCM aliyepata kura 1,205, Grace Ngalaba(CUF) alipata kura 12 na Emmanuel Mwasilembo(DP) kura 2.

Katika Kata ya Milongodi Wilaya ya Tandahimba, Manzi Livedo (CCM) ameshinda kwa kura 827, akifatiwa na Juma Mngawa (CUF) kura 819.

Kata ya Mnacho wilayani Ruangwa, Damian Chilemba (CCM) 1,924 na Onesmo Kambona (Chadema) 637.

Kata ya reli Wilaya ya Mtwara, Genfrid Mbunda (CCM) 422 Antony Kwezi (Chadema) 356, Mwajuma Hassan (ACT) 27 na Phillipo Mwomba (CUF) 21.

Kata ya Chanikanguo Halmashauri ya mji Masasi, Nichalaus Syprian (CCM) 928, James Kaombe(Chadema) 773, Musa Nangoha (CUF) 36 na Humphrey Kasembe(ACT) 10

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search