Wednesday, 22 November 2017

CLOUDS MEDIA YAPIGWA FAINI MILION 12 KWA KIUKA MAUDHUI YA UTANGAZAJI

Mamlaka  ya udhibiti wa mawasiliano nchini (TCRA) imekitoza kituo cha redio cha Clouds FM faini ya shilingi milioni 12 ikiwa ni pamoja na kupewa onyo kali kwa sababu ya kukiuka maudhu na kanuni za utangazaji kupitia vipindi vya Jahazi na XXL.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  jijini Dar, Makamu  Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema Clouds FM imetozwa shilingi milino tano kwa kosa la kukiuka misingi na maudhui ya utangazaji kupitia kipindi cha Jahazi kwenye kipengele cha Mastori ya Town, shilingi milioni tano kupitia kipindi cha Jahazi kipengele cha Najua Wajua na shilingi milioni mbili kupitia kipindi cha XXL.

“Hata hivyo, tunaitaka Clouds Media Group kuwaomba radhi wasikilizaji wa vipindi hivyo kwa siklu tatu mfululizo na pia tunautaka uongozi wa Clouds Media Group kuwachukulia hatua za kinidhamu watangazaji wanaokiuka maadili, miiko na kanuni za utangazaji,” alisema Mapunda VIDEO:


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search