Wednesday, 1 November 2017

DIAMOND PLATNUMZ:SINA UWEZO WA KUMLIPA HAMISA MOBETO MIL KWA MWEZI

Msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz, amedai mahakamani kuwa hana uwezo wa kumlipa Mwanamitindo Hamisa Mobeto, Sh milioni tano kama gharama za matunzo ya mtoto kwa mwezi.


Diamond amewasilisha majibu hayo katika Mahakama ya Watoto Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobeto kumfungulia kesi ya madai katika Mahakama hiyo ya watoto akidai mambo mbalimbali ikiwamo matunzo ya mtoto.


Katika majibu yake Diamond amedai fedha hizo anazodai Hamisa kulipwa kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.


Mobeto katika maombi yake kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck wa Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys, anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, mtoto huyo wa kiume aliyezaa na msanii huyo na kumuomba msamaha kwa umma kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.Baada ya kupokea majibu hayo mahakama iliahirisha kesi hiyo ya madai hadi Novemba 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mobeto kupitia wakili wake walimpa notisi Diamond ya kutaka amwombe radhi na kupeleka matunzo ya mtoto ndani ya siku saba lakini notisi hiyo haikutekelezeka hivyo aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search