Monday, 27 November 2017

GARI AINA YA NOAH NA HIACE ZIMEGONGANA NA KUUA WATU KUMI NA MBILI

Muonekano wa Hiace baada ya ajali
Muonekano wa Noah baada ya ajali


***

Watu 12 wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Hiace yenye usajili namba T.581 BBV waliyokuwa wakisafiria kutoka kumchukua Bibi Harusi kugongana uso kwa uso na Toyota Noah yenye namba T.423 CFF iliyokuwa imepakia watu kutoka msibani katika ajali iliyotokea kijiji cha Ighuka wilayani Ikungi kwenye barabara kuu ya Singida – Manyoni .Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Debora Magiligimba amesema kuwa ajali hiyo imetokea Jana Novemba 23,2017 Alhamis majira ya saa 2.30 usiku ikihusisha Toyota Hiace iliyokuwa ikitokea Singida kwenda Manyoni na Noah iliyokuwa ikitokea Manyoni kwenda Singida.Malunde1 blog imeambiwa  kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa Hiace ambaye alihama upande wake na kugongna uso kwa uso na Noah hiyo watu 10 walifariki papo hapo na majeruhi wawili kati ya 24 waliofikishwa Hospitali ya Misheni Puma kwa ajili ya matibabu pia waliofariki, hivyo kufanya idadi ya waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo kufikia 12.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search