Thursday, 9 November 2017

GODBLESS LEMA-''MAGUFULI NI MPANGO WA MUNGU''

Image result for godbless lema
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amekiri kwa wakazi wa Murieti Mkoani Arusha kwamba Rais John Magufuli ni Mpango wa Mungu kwani Mpango wa Mungu siyo lazima uwe mzuri.

Akizungumza wakati wa kumuombea kura mgombea wa udiwani kata ya Muriet, Mh. Lema amesema kwamba maisha watanzania wanayoyapitia ni kutokana na serikali ya awamu ya tano.
"Rais Magufuli mimi nasema ni Mpango wa Mungu. Ugumu huu wa Maisha umesababishwa na serikali ya awamu ya tano wafanyabiashara hawana kazi, hivyo ninaposema ni mpango wa Mungu mkumbuke siyo lazima uwe mzuri lakini pia naombeni nikisema mpango wa Mungu mjue anawakumbusha nini cha kufanya" Lema.
Mh Lema katika Kata hiyo ambaye amemnadi mgombea Mosses amesema kwamba vitisho vya Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo haviwashtui kwani yeye anachojua ni kwamba CHADEMA itashinda na wao watashindwa hivyo mpango wa kugoma klumtangaza mshindi wa cchadema utawapa nafasi ya kutambua namna ya kuishi nao wakati mwingine.

Pamoja na hayo Mbunge Lema amewataka wananchi wa Murieti kumpigia kura mgombea huyo wa Chadema Simon Moses Mollel. kwani ndiye atakayeweza kuwatetea katika kutafuta maendeleo na siyo CCM ambayo imekuwa ikisababisha maisha magumu.

Hata hivyo Lema amewaweka wazi wana Muriet kwamba pamoja na kuwa bunge limekwishaanza hataweza kuondoka mkoani hapo mpaka atakapohakikisha amewachosha CCM vya kutosha.

EATV

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search