Thursday, 9 November 2017

HOTEL YA BLUE PEARL YAFUNGWA KWA KUDAIWA KODI YA BIL 5.7


Habari zilizotufikia ni kwamba Kampuni ya udalali ya Yono asubuhi ya leo November 9, 2017 imeifunga Hotel ya Blue Pearl iliyopo kwenye jengo la Ubungo Plaza eneo la Ubungo kutokana na mmiliki wake kudaiwa kodi ya pango Tshs bilioni 5.7.

Mpaka muda huu baadhi ya wageni waliokuwa wako hotelini hapo wameanza kutolewa kutokana na kufungwa kwa hoteli hiyo.

Inaelezwa pia kuwa magari zaidi ya 20 yanayomilikiwa na hoteli hiyo nayo yamefungwa kutokana na mmiliki kudaiwa kodi hiyo ya pango na tayari kampuni hiyo ya udalali imekwisha anza kufuta maandishi ya ‘Blue Pearl Hotel’ kwenye mlango wa kuingilia.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search