Wednesday, 22 November 2017

JENGO LA CLOUDS MEDIA LAUNGUA MOTO

Habari kutoka jijini Dar es salaam zinasema kuwa sehemu ya jengo la Clouds Media limeungua moto.

Moto huo umezuka katika ofisi za Clouds Media Group na kusababisha Television na Radio Clouds kutokuwa hewani kwa muda.

Moto huo ulianza saa 4 asubuhi leo Jumanne Novemba 21,2017 katika chumba kimoja kwenye ghorofa ya kwanza uliosambaa kwenye jengo la kampuni hiyo.

Taarifa za awali zinasema moto huo umetokana na hitilafu ya umeme kwenye chumba cha kurushia matangazo cha Clouds TV.
Magari ya Zimamoto yapatayo manne yalifika eneo la tukio kwa ajili ya kuzima moto huo.

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds, Ruge Mutahaba amesema amewashukuru Zimamoto kwa kuweza kuokoa vifaa na kuzima moto huo

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search