Friday, 24 November 2017

JESCA KISHOA :-MME WANGU AMEINGIA KWENYE KUNDI LA WANASIASA WASIO NBA MSIMAMO

Mke wa aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, Jesca Kishoa, amemtaja mumewe kuwa ni mtu aliyeingia kundi la wanasiasa wasio na msimamo.

Kishoya amesema wakati wote mumewe amekuwa na msimamo usioyumba lakini anashangazwa kaingia katika mtego mbovu.

"Bado naamini kuwa Chadema ni mahali sahihi kabisa ambapo siwezi kufikiri siku moja nitatoka, hivyo siyumbi kwa hilo na wanaonipigia simu watambue hilo," amesema Kishoya

Amesema taarifa za mumewe kujiondoa Chadema amezipata kupitia vyombo vya habari akiwa Dodoma kwenye kampeni za udiwani lakini alimpigia wakazungumza sana na bado hakumpa sababu zilizoshiba za kuondoka kwake.

Hata hivyo amepinga madai ya Kafulila kuwa anaondoka upinzani kwa sababu ya upinzani kushindwa kusimamia ajenda ya ufisadi badala yake akasema ana mambo yake.

"Wanasiasa ambao hawana misimamo ndiyo husingizia vitu hivyo, siamini kama maneno yale yalitoka rohoni mwake, CCM siyo mahali sahihi kwa kuzungumzia mambo ya ufisadi hata kidogo, "

Mbunge huyo amesema wakati wote katika maisha yao mumewe amekuwa ni muumini mzuri wa kuhubiri habari za ufisadi ikiwemo pale alipotoa maisha yake kuhusu sakata la Escrow.

Na Habel Chidawali, Mwananch

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search