Thursday, 2 November 2017

Mahakama ya Juu Yasitisha Uchaguzi wa Rais Liberia

Mahakama ya Juu Yasitisha Uchaguzi wa Rais Liberia


Mahakama ya juu zaidi nchini Liberia imeamrisha maandalizi ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais kusitishwa kufuatia madai ya udanganyifu kutoka kwa mgombea aliyeondolewa kutoka kinyanganyiro hicho.
Mcheza soka wa zamani George Weah na makamu wa Rais Joseph Boakai wanatarajiwa kukutana katika duru hiyo ya pili ya tarehe 7 Novemba.
Lakini mgombea wa chama cha Liberty Charles Brumskine, ambaye alichukua nafasi ya tatu amepinga matokeo hayo.
Uchaguzi Liberia: Weah na Boakai kuelekea duru ya pili ya uchaguzi wa rais
Aliyekuwa mke wa Charles Taylor kujibu mashtaka Uingereza
Uchaguzi wa mwezi uliopita ndio wa kwanza huru kufanyika tangu kukamilika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003.
Mahakama imeamrisha chama cha Liberty na tume ya uchaguzi nchini humo kupeleka kesi zao ifikapo Alhamisi.
Lakini msemaji wa tume ya uchaguzi Henry Flomo aliambia BBC kuwa hajajulishwa rasmi kuhusu amri hiyo ya mahakama.
Waangalizi wa kimataifa wakiwemo wale kutoka muungano wa Ulaya hahawajaelezea hitilafu yoyote wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search