Thursday, 23 November 2017

MAMBA MWEUPE AONEKANA NCHINI AUSTRALIA

Ni nadra kumuona mamba wa aina hiyo eneo la mwituni kama si mwenye umri mdogo, anasema mtaalam.

Kuonekana kusiko kawaida kwa mamba mweupe mwenye umri mkubwa kumewasisimua wanaofanya shughuli za utalii katika eneo la Kaskazini mwa Australia.

Mnyama huyo wa jamii ya wanyama watambaao , aliyepewa jina la bandia -Pearl, alionekana katika ziwa Adelaide River katibu na eneo la Darwin siku ya Jumapili

Mtu mmoja aliyemuona, ambaye ni mwanaharakati wa hifadhi ya mazingira , alikadiria kuwa mamba huyo alikuwa na urefu wa mita takriban 3 za urefu.

Muonekano wa weupe wa rangi wa mnyama huyo umetokana na hali ya hypomelanism - inayosababishwa na ukosefu wa madini ya mwili yanayotengeneza ngozi melanin, kulingana na wataalam wa masuala ya wanyama..

Wakazi wa eneo lililo karibu na mto Adelaide wanaamini mnyama huyo ana uhusiano na mamba mwingine anayefahamika kuwa na hali hiyo ya afya ya mwili ambaye aliwahi kumuua mvuvi mnamo mwaka 2014.

"Kila mmoja anaelezea furaha yake ," alisema rais asiye rasmi wa kikundi cha uhifadhi wa mazingira katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja kama Broady.

"Nilishinda siku nzima nikitokwa na machozi ya furaha nikimtazama."

Ni Kwanini mamba ni mweupe?

Wengi miongoni mwa mamba nchini Australia wanarangi za kijivu na kijani, jambo linalowawezesha kutoonekana kwa urahisiMamba alishuhudiwa na muongozaji wa watalii katika eneo la kaskazini mwa Australia

Hitilafu ya kimwili ya Mamba Pearlhuenda ilistokea kupitia Jeni ama wakati wa kutengenezwa kwa yai , alisema Adam Britton, mtafiti msaidizi katika chuo kikuu cha Charles Darwin University.

"Wakati wa kutotoa kama mayai yatakuwa moto zaidi kiasi , inaweza kusababisha hitilafu katika kitengo cha seli na hivyo kusababisha kumeguka ," Alisema Bwana Britton.

Alisema matokeo yake yanaweza kuwa ni pamoja na "kuondolewa kwa rangi ya mwili au sehemu nyingine ya magamba kwenye mwili ".

Ni hali ya nadra ?

Mamba hao si " ni wa kawaida kuonekana'' wakiwa na umri mdogo wanapokuwa na umri mdogo, hususan katika hifadhi ya mamba, kwa mujibu wa Bwana Britton.

However, it is difficult for a pale juvenile to steer clear of predators.Mamba alipewa jina la bandia Pearl na wakazi

"Ni jambo lisilo la kawaida kidogo kumuona mamba mwenye umri mkubwa akiwa na rangi nyeupe kiasi hicho ," Bwana Britton alisema.

"Nimeisha waona mamba kama huyu kila mara, lakini si mkubwa kiasi hiki mwituni.

Chanzo-BBC

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search