Wednesday, 29 November 2017

MMILIKI WA SHULE YA SCHOLASTICA APANDISHWA KIZIMBANI

Mmiliki wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Scolastica iliyopo mji wa Himo wilayani Moshi,mkoani Kilimanjaro Edward Shayo amefikishwa mahakamani leo Jumatatu kusomewa shitaka la mauaji.


Mmiliki huyo, pamoja na watu wengine wawili wanatarajiwa kusomewa shitaka la mauaji ya mwanafunzi wa shule hiyo, Huphrey Makundi (16) aliyekuwa kidato cha pili.


Shayo ametolewa hospitali ya rufaa ya KCMC alikolazwa na kupelekwa moja kwa moja Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi chini ya ulinzi mkali wa polisi.


Muda wowote kutoka sasa anatarajiwa kusomewa shtaka hilo pamoja na mlinzi wa shule na mwalimu mmoja ambao tayari nao wapo chumba cha mahabusu cha Mahakama.


Mtoto huyo alitoweka shuleni Novemba 11 na baadaye kubainika ameuawa baada ya maiti yake iliyozikwa kama ya mtu asiyefahamika, kufukuliwa Novemba 17.
Chanzo-Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search