Monday, 13 November 2017

MTU MMOJA NCHINI INDIA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI AKISAFIRISHA NG'OMBE ANAYEAMINIWA KUWA NI MUNGU

Viongozi wa kijamii katika mji wa Rajasthan nchini India wanasema mtu mmoja ambaye ni muislam ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaoamini ng'ombe kuwa mungu wao.

Ummar Khan alikua akisafirisha ng'ombe yeye na mwenzake katika kitongoji cha Alwar wakati walipovamiwa na wahindu.

Wanasema kwamba mwili wa kijana huyo ulitupwa karibu na reli kuharibu ushahidi.

Polisi katika mji wa Rajasthan wameanzisha upelelezi juu ya tukio hilo.Umekuwa ni utamaduni wao tokea enzi na enzi

Wahindu huamini kuwa ng'ombe ni mungu kwao na huwachukulia kwa namna ya upekee sana.

Zaidi ya watu kumi wameuawa tokea mwaka 2015 kwa sababu kama hizo.

Chanzo-BBC

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search