Friday, 17 November 2017

MUGABE AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA JESHI PAMOJA NA UJUMBE WA AFRIKA YA KUSINI

Picha za kwanza za mkutano kati ya Rais Robert Mugabe na mkuu wa majeshi ya Zimbabwe Jen Constantino Chiwenga pamoja na wajumbe kutoka Afrika Kusini katika ikulu ya rais Harare zimetolewa.

Gazeti la Serikali la Herald limepakia picha hii kwenye Twitter:


BREAKING: President Mugabe meets ZDF Commander and SA envoys at State House . 
picha zingine hizi hapa
Mugabe (wa pili kulia) akiwa kuzuizi cha nyumbani akisimama na mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga (kulia)
Robert Mugabe alikutana na mkuu wa majeshi aliyeongoza hatua dhidi yake

Reuters Mugabe amekuwa akizuiliwa na wanajeshi nyumbani kwake Harare

Serikali ya Afrika Kusini imesema Rais Robert Mugabe anakutana na wajumbe kutoka nchi za kanda ya kusini mwa Afrika katika juhudi za kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Alisafiri hadi kwenye ikulu kutoka makao yake ya kibinafsi ambako amekuwa akizuiliwa na jeshi.

Wanajeshi waliingilia kati na kutangaza kudhibiti serikali Jumatano katika kinachoonekana kuwa juhudi za kumzuia mke wa Mugabe, Grace, asitwae madaraka.

Duru zinadokeza wkamba Bw Mugabe anataka kusalia madarakani hadi wakati wa kufanyika wka uchaguzi mwaka ujao.

Lakini mpinzani wake wa muda mrefu Morgan Tsvangirai amemtaka ajiuzulu mara moja kwa maslahi ya raia.

Makamu wake wa zamani Joice Mujuru pia ametaka kuwe na serikali ya mpito na pia uchaguzi huru na wa kuaminika.

Mzozo wa Zimbabwe pia unajadiliwa katika mkutano wa jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC, nchini Botswana. 

Joice Mujru, makamu wa rais wa zamani na kiongozi wa muungano wa upinzani wa People's Rainbow Coalition (PRC), ameomba kuwepo na mazungumzo yanayoshirikisha wahusika wote nchini humo.

Amesema matokeo ya mazungumzo hayo inafaa kuwa uchaguzi huru na wa haki Zimbabwe.

Amani inaweza tu kupatikana kwa kuvumiliana na kubadilishana mawazo kwa Wazimbabwe wenyewe. Tukisonga mbele … matukio ya kisiasa yanahitaji kuhusisha wadau wote muhimu humu nchini.

Shughuli ya kujenga upya nchi yetu na kuhakikisha maridhiano ya taifa inaweza tu kutokea iwapo kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki, ambao utafanyika kwa kipindi kifaacho na kitakachoafikiwa wakati wa kuunda serikali ya mpito.

Kabla ya kufutwa kazi kwake mwaka 2014, Bi Mujuru alitazamwa na wengi kama mrithi mtarajiwa wa Bw Mugabe.

Hata hivyo alifukuzwa kutoka kwenye chama tawala mwaka 2015.

Mwezi uliopita, alichaguliwa kuwa kiongozi wa muungano wa vyama sita vya upinzani kwa jina People's Rainbow Coalition. 

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe Morgan Tsvangirai amesema Rais Robert Mugabe anafaa kujiuzulu mara moja na kupisha serikali ya mpito ambayo itafanikisha kuandaliwa kwa uchaguzi huru na wa kidemokrasia.


Tsvangirai amesema hayo akihutubia wanahabari mjini Harare.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search