Wednesday, 22 November 2017

MWENYEKITI WA BAVICHA KATROBAS KATAMBI AHAMIA CCM

Mwenyekiti wa baraza la Vijana Chadema taifa (BAVICHA),Patrobas Katambi amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM). 
Katambi ametangaza kujiondoa Chadema leo Jumanne Novemba 21,2017 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kinaoendeshwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam. 

Katambi alikuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 akikabiliana na Stephen Masele (CCM) ambaye aliibuka mshindi huku Katambi akidai kuibiwa kura katika uchaguzi huo. 

Akizungumza katika kikao hicho Patrobas Katambi alisema kama ataitwa msaliti basi atakuwa kundi la wasaliti wa nchi hii. 

“Mambo mengi yalikuwa mrama na watu tunapenda mabadiliko ila hatutaki kubadilika, kama nitaitwa msaliti basi nitakuwa msaliti kundi la wasaliti wa nchi hii, ukombozi ulishapatikana, siyo tunachokisema majukwaani ndiyo tunachokiishi",alisema Katambi. 


"Maisha tunayoyahubiri siyo tunayoishi, ukienda jimboni kwake, vijana kama nguvu kazi ya taifa, tunajadili ‘personalities’ badala ya ‘issues’ mawazo mbadala,niwaombe nijiunge na CCM siyo kwa sababu za madaraka ila tuijenge, CCM inatoa nafasi kwa vijana, vijana kwa upinzani ni sawa na karai katika ujenzi”,aliongeza Katambi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search