Thursday, 9 November 2017

NDEGE YATUA KWA DHARURA NCHINI INDIA KUFUATIA MKE KUMFUMANIA MUMEWE

Ndege Yatua kwa Dharura Baada ya Mke Kumfumania Mumewe
Ndege ya Qatar Airways ambayo ilikuwa ikitokea Doha kuelekea Indonesia ililazimika kutua kwa dharura India usiku wa manane kufuatia abiria mmoja mwanamke kuanza kumpiga mumewe akimtuhumu kumsaliti baada ya kufungua simu ya mumewe huyo wakati amelala.

Unaambiwa simu ya mume huyo ilikuwa na password ya fingerprints ambapo mwanamke huyo alitumia kidole cha mumewe akiwa amelala na kuifungua simu na kugundua mumewe huwa anamsaliti.
Baada ya vurugu hizo kuendelea Ndege ilitua Chennai, India kwa dharura kisha wakaamriwa kuteremka na kuwekwa kizuizini katika Airport kabla ya kusafirishwa kuelekea Kuala Lumpur

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search