Monday, 27 November 2017

NDEMLA AFUZU MAJARIBIO NCHINI SWEDEN

 
 
Klabu ya Simba imetoa taarifa kuhusu kiungo wake Said Ndemla kufuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya. Taariga kamili ya Simba hii hapa:
 
Simba Sports Club
Dar es salaam
25-11-2017. 
            TAARIFA KWA UMMA
Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya. 

Ndemla aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya huko.anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu inayokuja. 

Na mara baada ya kurejea. klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko. 

Kiufupi klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi, na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla. 

Wakati huo huo kesho klabu ya Simba itakutana na viongozi wote wa matawi.

Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa tarehe 3-12-2017. na mkutano huo wa kesho utafanyika makao makuu ya klabu kuanzia saa Nne kamili asubuhi ya jumapili ya tarehe 26-11-2017.

Mwisho
Uongozi wenu unawaomba Wanachama na washabiki wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Uhuru kuishangilia timu yao, itakapocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Lipuli ya Iringa. 

HAJI S. MANARA

Mkuu wa Habari  na mawasiliano Simba  Sports Club.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search