Thursday, 2 November 2017

NYALANDU AMTEMBELEA TENA LISSU HOSPITALINI NAIROBI ALIKO LAZWA

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini ambaye amejiuzulu nafasi yake hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lazaro Nyalandu amemtembelea tena Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu jijini Nairobi Kenya ambapo anapatiwa matibabu na kumuombea.

Lazaro Nyalandu alipotangaza kujiuzulu nyazifa zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua ya kujiuzulu Ubunge wake kwa Spika wa Bunge Job Ndugai alifunga safari na kwenda nchini Kenya, ambapo huko alipata nafasi ya kumtembelea Mbunge Tundu Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.

"Mungu akuangazie nuru za uso wake na kukupa amani kaka yetu mpendwa Tundu Lissu.

Akakuponye majeraha na maumivu yako na kukufanya Taifa kubwa. Kwa wote wanakuombea na kukupenda, ikawe heri kwao, na kwako iwe amani, uponyaji na mafanikio. Utukufu ujao uwe Mkuu kuliko ule wa awali" alisema Lazaro Nyalandu

Mbunge Tundu Lissu bado yupo nchini Kenya jijini Nairobi akipatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Dodoma.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search