Thursday, 23 November 2017

NYUMBA ZA LUGUMI KUUZWA TENA KESHO

 Nyumba za Dkt Shika Kuuzwa kwa Mara Nyingine Kesho
NYUMBA mbili za Lugumi ambazo hazikufanikiwa kuuzwa katika minada iliyopita, zitauzwa kwenye mnada utakaofanyika kesho jijini Dar es Salaam maeneo ya JKT Mbweni na Upanga.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kevela, alipozungumza na vyombo vya habari ambapo alitoa onyo pia kwamba watu wasiokuwa na nia ya kununuanyumba hizo wasifike sehemu hizo kwani watachukuliwa hatua.

Alirudia kusisitiza kwamba watu watakaofanikiwa kununua nyumba hizo ni lazima watangulize asilimia 25 ya bei husika na iliyobaki ilipwe ndani ya siku 14 la sivyo fedha iliyotangulizwa haitarudishwa

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search