Saturday, 11 November 2017

RAIS HUYU AKUMBWA NA KASHFA YA NGONO

Golikipa wa timu ya soka ya wanawake ya Marekani Hope Solo, amejitokeza na kuweka wazi kwamba amewahi kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter.

Solo mwenye miaka 36 ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia kwa wanawake, ​​amesema tukio hilo lilitokea katika tuzo za Ballon d'Or za 2013 wakati akijiandaa kwenda kukabidhi tuzo kwani alikuwa ni miongoni mwa watu waliokabidhiwa jukumu hilo.
Katika mahojiano na gazeti la Expresso la Ureno, Solo amesema alikuwa nyuma ya jukwaa akiwa tayari kwaajili ya kukabidhi tuzo lakini aliitwa na rais Blatter kwenye kaunta binafsi kisha akaanza kumpapasa makalio.

Hata hivyo Blatter mwenye umri wa miaka 81, kupitia kwa msemaji wake amekanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na ni upuuzi ambao unalenga kumchafua.
Siku za hivi karibuni kumekuwepo na ripoti nyingi za wanawake kunyanyaswa kijinsia hususani kwenye kiwanda cha filamu cha Hollywood nchini Marekani. Hata hivyo Solo ameongeza kuwa sio tukio hilo pekee bali unyanyasaji huo ni vitendo vilivyokisili kwenye soka la wanawake

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search