Thursday, 23 November 2017

RAIS MATARAJIWA WA ZIMBABWE AWASILI JIJINI HARARE

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerudi nchini humo kutoka Afrika Kusini.

Anatarajiwa kutoa hotuba yake katika makao makuu ya chama cha Zanu-PF mjini Harare.

Awali Mnangagwa amekutana na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Bwana Zuma alitarajiwa kuwasili atika mji mkuu wa Harare leo ili kuwa mpatanishi wa mgogoro uliokuwa ukiendelea lakini akafutilia mbali zaiara hiyo baada ya rais Mugabe kujiuzulu.


Ofisi ya rais Zuma ilituma ujumbe wa Twitter wa picha za mkutano wao.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search