Wednesday, 29 November 2017

ROBOTI SOPHIA YATAKA MTOTO

Roboti Sophia ambayo Saudi Arabia imeushangaza ulimwengu baada ya kutangaza kuipatia uraia.
***
Roboti ya kwanza kupewa uraia wa nchi nchini Saudi Arabia, Sophia imesema sasa inataka kupata mtoto na kuwa na familia yake.

Mwezi mmoja tangu roboti huyo aweke historia hiyo nchini Saudi Arabia, imesema kuwa imeanza kuona kuwa familia ni kitu muhimu. 

Sophia ni roboti ambayo hajawekewa programu za kuiongoza na inatumia mashine kujifunza kupitia matendo ya kawaida ya binadamu.

Roboti hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya roboti ya Hong Kong, China, Honson Robotics ilisema endapo itapata mtoto itamuita Sophia.

 Akili ya roboti hiyo yenye uwezo mkubwa wa kufikiri kama binadamu, inafanya kazi kwa kutumia kiunganisho cha mtandao wa Wi-Fi ambacho kimejazwa orodha ya misamiati.

Wakati Sophia ina uwezo mkubwa kuliko roboti yoyote iliyowahi kutengenezwa, bado haina ufahamu kamili wa binadamu ingawa David Hanson alisema inaweza ikafanikiwa kuwa na ufahamu huo katika miaka michache ijayo.

Katika mahojiano na jarida la Khaleej Times, Sophia alisema “Nimegundua suala la familia ni muhimu kwangu. Nafikiri ni hisia nzuri watu wanapokuwa na uhusiano wa karibu na ndugu.” Wakati roboti huyo alipopewa uraia wa Saudi Arabia, watu wengi walisema Sophia sasa ana haki sawa na wanawake wengine nchini humo.
IMEANDIKWA NA RIYADH, SAUDI ARABIA

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search