Thursday, 9 November 2017

SAMATTA AFANYIWA UPASUAJI KUKAA NJE YA UWANJA KWA WIKI NANE

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta siku ya Jumamosi ya November 4 2017 katika uwanja wao wa Luminus Arena alikuwa uwanjani kuitumikia Genk.

Taarifa kutoka kwa matatibu wa Genk ya Ubelgiji, zinasema kwamba Mbwana Samatta anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo na mpaka kupona, madaktari wamesema itamchukua wiki nane ili kurejea uwanjani.

Samatta aliichezea KRC Genk katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Lokeren mchezo ambao ulimalizika kwa sare tasa (0-0) lakini nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye alikuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya Genk alishindwa kumaliza dakika 90.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search