Tuesday, 7 November 2017

SERIKALI HAKUNA TATIZO LA DAWA NCHINI


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hakuna tatizo la dawa nchini kwani serikali imewekeza fedha nyingi kuhakikisha kuwa zinapatikana muda wowote.

Ametoa majibu hayo leo Jumanne Novemba 7,2017 wakati akimjibu mbunge wa Siha katika kipindi cha Maswali na Majibu cha Bunge la Tisa mjini Dodoma, Dk Godwin Mollel aliyetaka kujua hatua inayochukua serikali kukabiliana na upungufu wa dawa.

Waziri Ummy alisema kuwa wilaya zote, ikiwemo Siha, kuna dawa dawa zote 135 muhimu na kumtaka kuachana na taarifa zilizopitwa na wakati. Hata hivyo, Ummy ameongeza kuwa kati ya dawa zinazoagizwa, ni asilimia chini ya tano tu zinazoharibika, jambo ambalo linaendana na viwango vya kimataifa. “Sababu ya kuharibika kiasi hicho ni kuwa mahitaji halisi ya dawa hayawasilishwi,” ameongeza Waziri huyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search