Monday, 6 November 2017

SIMBA YARUDI KILELENI MWA LIGI KUU

Simba Yatimiza Ahadi Yake, Yarejea Kieleni


Klabu ya soka ya Simba imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Mbeya City jioni ya leo.

Simba ilifanikiwa kupata bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa Shiza Kichuya dakika ya 7 akipokea pasi safi ya Jonas Mkude ambaye leo ameanza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza msimu huu.
Bao la Kichuya lilifanikiwa kudumu kwa dakika 45 za kwanza pamoja na kuwepo kwa mashambulizi ya hapa na pale kwa timu zote mbili, lakini umakini wa walinda milango Aishi Manula wa Simba na Fikirini Bakari wa Mbeya City uliwanyima nafasi ya kufunga washambuliaji wa timu hizo.
Simba sasa imefikisha alama 19 na kupaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiishusha hadi nafasi ya pili timu ya Azam FC yenye alama 19 pia zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Baada ya mchezo wa leo raundi ya 9 imekamilika ambapo ligi itasimama kidogo kupisha kalenda ya shirikisho la kimataifa la soka FIFA, ambapo timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars itasafiri kucheza na Benin.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search