Thursday, 9 November 2017

Sitotaka tena kuwa na mwanume Tanzania:-Chuchu Hancy

Muigizaji wa filamu bongo Chuchu Hansy ambaye pia ni mzazi mwenzake Vicent Kigosi (Ray) amesema iwapo akiachana na Ray hatokuwa na mwanaume wa Tanzania tena.

Chuchu Hany ameyasema hayo alipokuwa akipiga Story na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba iwapo ataachana na mwenza wake huyo, hatakuwa kwenye mahusiano tena na mtu yeyote hususan wa hapa Tanzania.

"Kuachana kupo kwa sababu kila kitu Mungu ndio anapanga, kwa hiyo mimi siwezi kushindana na Mungu, kama ikitokea itakuwa imefikia mwisho wetu, sidhani kama nitakuwa tena na mwanaume tena hapa Tanzania, sidhani, yaani sijui kama nitaingia kwenye mahusiano, nitakaa muda mrefu bila mahusiano", amesema Chuchu Hansy.

Pamoja na hayo muigizaji huyo amekanusha tetesi za kuachana na mzazi mwenzake Ray Kigosi, baada ya kuwa na tetesi kuwa wawili hao wameachana.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search