Thursday, 23 November 2017

TAARIFA YA KLABU YA YANGA KUHUSU SUALA LA MISHAHARA YA WACHEZAJI

KLABU ya Yanga ambayo ndiyo mabingwa wa soka nchini kupitia kwa katibu wake mkuu wamethibitisha kumalizana na masuala ya Mishahara kwa wachezaji wake jambo ambalo lilikuwa likisemwa sana japo Uongozi wa Klabu hiyo ulikuwa ukilificha.


Mkwasa ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani wa Yanga na sasa akiwa kama katibu mkuu wa Klabu hiyo jana akiongea na EFM amethibitisha kuwa Wamemalizana na wachezaji waliokuwa wakiwadai mishahara na hakuna mchezaji anayewadai kwasasa na kuhakikisha hilo aliwataka kuwauliza wachezaji wa timu hiyo kama kuna madai ya mishahara.

Na mmoja wa watangazaji wa Kipindi Alithibitisha kwa kuongea na wachezaji wawili ambao majina yao hawakutaka yatajwe ambao wote walithibitisha kuwa mambo ya mishahara yamekaa sawa.


Kuna taarifa zilienea siku kadhaa kuwa wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara ya miezi miwili huku baadhi ya Taarifa zikienda mbali zaidi kwa kusema ni miezi mitatu hawajalipwa ila Taarifa nzuri ni kwamba kila kitu kiko sawa

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search