Thursday, 2 November 2017

UMEISIKIA HII:-WAKUTWA WAMEKUFA WAKIFANYA MAPENZI KWENYE TAXI .....MWANAMKE NI MKE WA MTU

Mwili wa mwanamke mmoja aliyeripotiwa kuwa ni mke wa mtu mwenye watoto wanne umekutwa kwenye taxi mjini Lagos, nchini Nigeria ukiwa juu ya kifua cha mwanaume ambaye naye alikuwa ameshakufa. 

Wote wawili wakiwa wamelaliana wakishiriki tendo la ndoa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea Jumapili ya wikiendi iliyopita wamesema walikuta gari dogo (Taxi) ikiwa imepaki na ndani kukiwa na watu waliokuwa uchi wakiwa wamelaliana ndipo wakaamua kuchukua uamuzi wa kufungua milango.

Shuhuda mmoja alikiri wazi kumfahamu mama huyo na kudai kuwa ameolewa na ana watoto wanne huku akishindwa kumtambua mwanamme aliyekuwa naye.

Baadhi ya maelezo ya mashuhuda kupitia mitandao ya kijamii wamesema walikuta gari na AC ikiwa imewashwa.


Hata hivyo hakuna taarifa rasmi kutoka jeshi la polisi nchini humo kuhusu tukio hilo la kusikitisha.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search