Thursday, 9 November 2017

VANESSA MDEE AMPA JUX MASHARTI HAYA ILI WARUDIANE

Good news ni kuwa Jux anaweza kupokelewa tena moyoni mwa Vanessa Mdee, bad news ni kuwa masharti ni magumu. Wawili hao walipokea shangwe za kutosha wikiendi kwenye show ya Fiesta mjini Morogoro baada ya Jux kutumia zaidi ya dakika 3 kumuimbia Vanessa wimbo ili warudiane.

Baada ya Jux kuimba kwa hisia hadi kupiga magoti, Vee ambaye alioneshwa kutoridhika, alimueleza masharti yake. “Huyu brother msimu wote wa Fiesta amekuwa akiniimbia sijui anauawa, sijui analia sielewi mimi,” alisema Vanessa huku uwanja ukilipuka kwa shangwe.

“Sasa sikilizeni,” aliendelea. “Nyie wote hapa ni mashahidi. Bado siamini kama anataka kurudiana na mimi. Nampa dakika 15 tu tukikutana Fiesta Dar es Salaam nyie ni mashahidi, akiweza fresh kama vipi aendelee kuuawa au sio?”

Jux alisema atazifanyia kazi dakika 15 hizo ili ampate tena mrembo huyo aliyeachana naye miezi michache iliyopita.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search