Thursday, 2 November 2017

Wakati Najiuzulu Nilifanya kwa Nia Yangu Sikuwa Nimepata Barua ya Kufukuzwa CCM- Nyarandu

Wakati Najiuzulu Nilifanya kwa Nia Yangu Sikuwa Nimepata Barua ya Kufukuzwa CCM- Nyarandu
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa hajawahi kupata barua yoyote kutoka CCM inayomfukuza unanacha kama inavyodai.

Mh. Nyalandu ameiambia Bongo5 kuwa ndani ya chama hicho huwa kuna utaratibu na hawamfukuzi mtu kwa barua bali kuna kuwa na vikao vinavyohusiana na maadili hivyo basi amesema tangu awe ndani ya chama hicho hakuna kikao kilichowahi muita kuhusiana na masuala ya maadili.

“Wakati najiuzulu tarehe 30 mwezi Oktoba, nilifanya hivyo kwa nia yangu mwenyewe na kwa uamuzi wangu mwenyewe, sikuwa nimepata barua yoyote kutoka CCM inayonifukuza, kwahiyo dhana ya kwamba kulikuwa na barua yakunifukuza uanachama sio kweli lakini vilevile ikumbukwe kwamba mimi sikuwa mwananchama wa kawaida mimi nilikuwa ni mbunge ana jimbo pili nilikuwa ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na utaratibu wa chama chetu haufukuzwi tu kwa barua huwa kuna vikao vinavyohusiana na maadili huwa vinakaa,” amesema Nyalandu.

“Hakuna kikao chochote tangu niwe mwananchama ambacho kiliwashawahi kuniita kuhusiana na masuala yanayohusiana na maadili, kwahiyo mimi naona tungejikita tu kufanya muktabari wa nchi yetu tufanye siasa za ushindani na turuhusu watu wawe huru na tusisababishe malumbano ambayo hayana sababu yoyote,”ameongeza.

Nyalandu Jumatatu hii ya tarehe 30 Oktoba mwaka huu aliamua kukihama chama cha Mapinduzi (CCM) na kujivua ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search