Thursday, 23 November 2017

WASANII 20 WAKATWA KWENYE FIESTA YA DAR

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Alhamisi hii katika kipindi cha Clouds360, amesema amepunguza wasanii 20 katika list ya wasanii ambao walipanga kuwepo kwenye show ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika viwanjwa Leaders Club.

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba

Ruge alisema miongoni mwa wasanii hao walioondolewa kisa muda ni pamoja na Lulu Diva, Zaiid, pamoja na ChinBeez.

‘’Tulikaa kama kamati jana tunatumia nguvu kubwa mno kwenye suala la muda wakati tuna shoo kubwa iliyokamilika, kwahiyo tumeamua kuachana na suala la muda,tumeamua tukae kwenye muda tulioupanga sisi na kuhakikisha tuna ‘six hours’ za entertainment ambazo zimepangwa na kupangika,” alisema Ruge.

Aliongeza, “Kitakachokosekana ni wale wasanii zaidi ya 20, kama, Bright, Mimi Mars,Lulu Diva, Zaiidyao, ChinBeez,hao bahati mbaya ni lazima tuwaondoe kwa sababu ya ratiba kubana kutokana na muda, tungeweza kuwaingiza lakini hatuna muda’

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search