Thursday, 2 November 2017

Waziri Mbarawa atofautiana na Makonda, ataka Magari ya Serikali yatengenezwe na TAMESA

  1. CA05C292-6335-4078-AD88-1A67E583DD4B.jpeg 


    Akizungumza leo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa asema kuwa, Magari yote ya Serikali yanapaswa kutengenezwa na WAKALA wa ufundi wa umeme (Tanzania Mechanical and Electronics Service Agency (TAMESA), kwani ndio wenye kazi ya kutengeneza.

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda Jumanne hii amekabidhi mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya DAR COACH LTD kwaajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.

    Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion moja fedha ya Serikali.

    RC Makonda amesema kuwa gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya siku 90 ambapo ameipongeza Kampuni ya DAR COACH LTD kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search