Wednesday, 8 November 2017

Waziri wa fedha: Deni la taifa limeongezeka kwa asilimia 17 ndani ya mwaka mmoja

Serikali kupitia wizara ya fedha imesema kuwa deni la taifa limeongezeka kwa asilimia 17 kutoka dola za kimarekeni milioni 22,000 mwezi Juni mwaka 2016 hadi kufikia dola za kimarekani milioni 26,000 mwezi Juni mwaka 2017.

Waziri wa fedha na mipango Dkt. Philipo Mpango amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na mwongozo wa maandalizi ya mapango wa bajeti kwa mwaka 2018/2019.

Kwa mujibu wa Dkt. Mpango deni hilo la taifa linajumuisha deni la serikali lililofikia dola za kimarekani milioni 22, 000 na deni la sekta binafsi.

Katika hatua nyingine Dkt. Mpango amesema kuwa licha ya ongezeko hilo viashiria vinaonesha kuwa bado deni la taifa ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, mrefu na wa kati.
Ongezeko hili limechangiwa na mikopo mipya iliyochukuliwa kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa reli kwa kiwango cha Standard Gauge, mradi wa Stratergic Cities na mradi wa usafirishaji Dar Es Salaam DART
Chanzo: Azam Tv

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search