Thursday, 23 November 2017

WAZIRI WA INDIA DHAMBI HUSABABISHA SARATANI

Himanta Biswa Sarma ni waziri wa afya wa jimbo la Assam
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHimanta Biswa Sarma ni waziri wa afya wa jimbo la Assam
Wahindi wameleezea hasira yao baada ya waziri kutoka jimbo la Assam kusema saratani " ni haki ya kiimani " inayosababishwa na " thambi mtu alizowahi kuzifanya ".
Himanta Biswa Sarma amesema kuwa watu pia wanaweza kupata ugonjwa kama saratani "kutokana na dhambi za wazazi wao".
Wagonjwa wa saratani na ndugu zao wamesema kuwa wamesikitishwa sana na kauli hiyo ya waziri.
Vyma vya upinzani vimeielezea kauli ya waziri huyo kama "bahati mbaya'', na wamemtaka aombe radhi kwa umma.
Chama cha upinzani jimboni humo cha All India United Democratic Front kimesema kuwa Bwana Sarma ametoa kauli hiyo ili ''kuficha udhaifu wake wa kudhibiti kusambaa kwa saratani jimboni''
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye tukio la umma katika eneo la Guwahati Jumatano.
"Mungu hutufanya sisi tuumie tunapotenda dhambi .Wakati mwingine tunaweza kukutana na vijana wadogo wenye maradhi ya saratani au mwanaume wenye umri mdopgo wanapata ajali. Ukichunguza kwa umakini maisha yao utabaini kuwa ni kwasababu ya madhambi yao . Hakuna kitu kingine . Lazima tupate haki kutoka kwa Mungu '', lilimnukuu gazeti la The Times la India.
Bwana Sharma, ambaye ni mwanachama wa chama tawala nchini India cha Bharatiya Janata Party (BJP), baadae alitoa tangazo la ufafanuzi kukanusha kauli yake , jambo lililowakera zaidi watu.
Chama cha (ICMR) kinasema kwamba ukosefu wa uelewa na njia za kupima maradhi ya saratani kumesababisha idadi ya wagonjwa wanaofika hospitalini kupima wakiwa na hatua ya mwanzo ya saratani kuwa asilimia 12.5% pekee.
Inakadiriwa kuwa idadi mpya ya visa vya ugonjwa wa saratani nchini India vitaongezeka kwa 25% ifikapo mwaka 2020, kwa mujibu wa ripot

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search