Thursday, 23 November 2017

ZIMBABWE KUSHUHUDIA DEMOKRASIA MPYA

Mnangagwa(Upande wa kulia) akiwa na Mugabe wakati wa enzi zao
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMnangagwa(Upande wa kulia) akiwa na Mugabe wakati wa enzi zao
Kiongozi mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema nchi yake kwa inashuhudia mwanzo wa demokrasia mpya.
Mnangagwa, ambaye anatarajia kuapishwa kushika wadhfa wa Urais wa nchi hiyo siku ya Ijumaa, amesema kipaumbele chake ni kujenga upya uchumi wa nchi hiyo na kuunda ajira mpya kwa idadi ubwa ya watu wasio na ajira.
Katika hotuba yake hiyo, aliyokolezwa na maneno yaliyokuwa yakitumika wakati wa vita vya uhuru wa nchi hiyo, Bwana Mnangagwa alilishukuru jeshi la nchi hiyo, ambalo liliingilia kati baada ya yeye kufukuzwa na Rais Robert Mugabe na kuweza kufanikisha hali iliyopo sasa kwa amani.
Makamu huyo wa Rais wa zamani anayesubiri kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo alirejea nchini Zimbabwe mapema jana.
Aidha alifahamisha kuwa aliikimbia nchi hiyo baada ya kutishiwa maisha yake baada ya kufukuzwa katika nafasi yake hiyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search