Monday, 18 December 2017

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA KUTOKA GHOROFA YA 62

Raia mmoja wa China, Wu Yongning anayependelea kuparamia na kuruka katika majengo marefu kutoka jengo moja kwenda jingine amefariki dunia baada ya kukosea hatua flani wakati akifanya kile anachopenda kufanya katika maghorofa.

Kijana huyo anayeparamia majengo makubwa bila ya vifaa vyovyote vya usalama hujirikodi video huku akishikilia mkono mmoja akining'inia kutoka juu ya mjengo hayo kwa vidole vyake tu vya mkononi.

Kilichofuata baada ya hapo ni jambo la kushtusha na la kusikitisha kwani raia huyo alianguka kutoka katika ghorofa ya 62 kutoka juu na kufariki papo hapo.

 Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza (BBC) maelfu ya wafuasi wake walishikwa na wasiwasi alipoacha kuweka video za vituko vyake katika mitandao kama vile Huoshan na Kuaishou, lakini kifo chake kilithibitishwa katika siku chache, kwanza na mpenzi wake baadaye likafuata tangzo la maafisa wa polisi.

Video ya kushtusha ya kilichoonekana kuwa muda wake wa mwisho wa uhai wake akiwa katika hekaheka za kuparamia kuta za majengo marefu katika mji wa Changsha city ilianza kusambaa katika mtandao wiki hii.

 Kifo chake kimezusha maswali mengi ya wasiwasi na ya kutafakari pamoja na mijadala mizito kuhusu kuhatarisha maisha katika kutafuta pesa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search