Monday, 18 December 2017

ALIYEKUWA RAIS WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA GRATIAN MUKOBA ANASWA KWA RUSHWA

 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma inamshikilia aliyekuwa Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Gratian Mukoba kwa tuhuma za kugawa rushwa kwa wajumbe wa chama hicho.


Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kuhanga amethibitisha kushikiliwa kwa Mukoba tangu saa tano asubuhi ya leo Jumamosi Desemba 16,2017.


"Ni kweli tunamshikilia tangu saa tano asubuhi, tunaendelea na uchunguzi na kama usipokamilika atalala," amesema.


Kuhanga amesema Mukoba amekamatwa katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma ambako kunafanyika uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi ikiwemo ya rais, aliyoiacha wazi baada ya kustaafu.


Nafasi nyingine ni katibu mkuu iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa akiishikilia Yahaya Msulwa kufariki dunia.


Mkutano wa CWT ulianza juzi na ulifunguliwa na Rais John Magufuli aliyeonya kuhusu matumizi ya fedha katika uchaguzi.


Rais Magufuli aliwataarifu walimu kuwa Takukuru ipo na inafuatilia uchaguzi huo.


Katika mkutano huo, Rais Magufuli alisema kuna mmoja wao aliwakimbia Takukuru mkoani Singida walipofuatilia tuhuma za ugawaji wa rushwa

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search