Wednesday, 13 December 2017

ALIYETUMBULIWA KWA VYETI FEKI AJIUA KAHAMA


Mkazi wa Majengo wilayani Kahama mkoani Shinyanga amejinyonga kwa kutumia kipande cha chandarua usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye chumba chake cha kupanga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugumu wa maisha.

Kwa mujibu wa kaka wa marehemu Said Ndago amesema kuwa mdogo wake ambaye amejinyonga anaitwa Jumnne Said Ndago  ambaye alikuwa ameachishwa kazi ya Udreva katika halmashauri ya Msalala kutokana na kutokuwa na vyeti.

Amesema kuwa kabla ya kujinyonga aliandika Meseji kwa dada yake ambaye anafanya kazi Jijini Dar es salaam ambayo ilikuwa inasema kuwa anamuomba amtunzie watoto wake kwani yeye hatakuwepo duniani .

Kwa upande wake jirani wa marehemu ambaye walikuwa wanaishi nyumba moja Edward Nkondi amesema kuwa kijana huyo hakuwa anashinda Nyumbani kutokana na kuwa mke wake wake alikuwa amekwenda kwao Tabora hivyo alikuwa anaishi Peke yake hali ambayo ilikuwa ikichangia kutoshinda Nyumbani.

Amesema kuwa alikuwa anafika kwake usiku , lakini pamoja na kufika kwake alikuwa haonyeshi dalili za kwamba angefanya tukio kubwa kama hilo alilofanya la kujinyonga na kwamba alikuwa kijana mcheshi na mchangamfu.


Naye mkuu wa kitenngo cha Upelelezi ndani ya jeshi la Polisi mjini Kahama George Bagyemu kwa niaba ya Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Simon Haule amekiri kupokea taarifa hiyo na kwamba tatizo la kujinyonga ni ugumu wa maisha .

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search