Wednesday, 13 December 2017

Hashim Rungwe Atinga Nairobi Kumjulia Hali Tundu Lissu

Hashim Rungwe Atinga Nairobi Kumjulia Hali Tundu Lissu
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe Spunda, amemtembelea na kumjulia hali mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu Hospitali Nairobi alikolazwa baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, Mjini Dodoma.

Akiwa Nairobi, Rungwe ambaye alikuwa miongoni mwa wagombea Urais Mwaka 2015, ametoa wito kwa Watanzania kuwa na moyo wa upendo huku akiliomba Jeshi la Polisi na vyombo vya Dola kufanya kila njia kuwapata waliomshambulia Lissu.

Lissu alikimbizwa katika hospitali hiyo baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Area D, Mjini Dodoma, Septemba 7 mwaka huu ambapo amefanyiwa upasuaji mara kadhaa na anaendelea na matibabu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search