Tuesday, 12 December 2017

HAYA NDIYO MANENO YALIYOSEMWA NA DR SHIKA BAADA YA BABU SEYA NA MWANAE KUTOKA GEREZANI

Dkt Shika Afunguka Ukweli Kuhusu Babu Seya
Dr. Luis Shika amesema hamjui mwanamuziki Babu Seya na Papii Kocha ambao wametoka jela kwa msamaha wa Rais wa  Jamhuri ya  Muungano  wa  Tanzania John Pombe  Magufuli katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika.

Dr. Shika amesema wakati Babu Seya anaingia nchini Tanzania  yeye alikuwa nje ya nchi hivyo hajawahi kumuona lakini anafahamu nyimbo zake ambazo aliwahi  kuimba.
''Simfahamu Babu  Seya, wakati anaingia nchini  tayari nilishaondoka nchini muda mrefu, lakini nafahamu nyimbo zake ile aliyoimba baba na mwana tunaimba na kucheza ndio haswa naifahamu vizuri'', amesema.

Pia Dr. Shika amempongeza Rais Magufuli kwa kuwatoa wafungwa mbali mbalimbali  na kutumia vizuri fursa ya uongozi kama mkuu wa nchi. ''Nampongeza Rais Magufuli kwa tukio hili la kuwatoa wafungwa  na kuwapa uhuru wakaanze maisha yao upya'', ameongeza.

Nguza Viking maarufu kama ''Babu  Seya'' na Johnson Nguza ''Papii Kocha'' walipatikana na hatia ya kubaka na kunajisi watoto na walihukumiwa kwenda jela maisha tangu mwaka 2004 kabla ya kupata msamaha mwaka huu wakiwa wamedumu gerezani kwa miaka 13.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search