Monday, 18 December 2017

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI AKIFUNGUA MKUTANO MKUU WA CCM


Magufuli akihitubia.
MKUTANO Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) umeanza Mjini Dodoma ambapo utafanyika  kwa siku mbili, Desemba 18-19, 2017 ambapo Mkutano huo  umebeba ajenda kuu ya kukamilisha uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaanza leo bila kuwa na shamrashamra zilizozoeleka katika mikutano iliyopita.

“Chama chetu kimedhamiria kutokomeza rushwa, ndiyo maana mlisikia juzi hapa tulifuta matokeo ya mchakato wa kumpitisha mgombea Ubunge wa CCM, Jimbo la Singida ya Kaskazini baada ya kuona kulikuwa na harufu ya rushwa katika mchakato huo.

“Tumepunguza idadi ya vikao na wajumbe wa vikao vya chama ili kupunguza gharama za uendeshaji. Tumefanya hivyo ili viongozi watumie muda mwingi kutatua matatizo ya wanachama na ya wananchi.

“Tumefuta utaratibu wa mtu mmoja kuwa na vyeo zaidi ya kimoja ndani ya chama, tumebadili katiba yetu ya chama, haya ndiyo mageuzi makubwa tuliyoyafanya ndani ya chama,” alisema Magufuli wakati akizindua mkutano huo.

“Viongozi waliochaguliwa mhakikishe mnaongeza wanachama hai kwenye maeneo yenu ili ikifika wakati wa uchaguzi tuwe na wanachama wa kutosha na hawa wapinzani wanaotutazama wasiambulie chochote
“Msichague watu kwa urafiki au kwa sababu ya rushwa, binafsi napenda nimshukuru mzee Kikwete (Jakaya) yeye hakuangalia rushwa nadhani angefanya hivyo huenda mimi nisingepita,” amesema.

Rais Magufuli amewataka wanachama wa CCM kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa chaguzi wa ndani wa chama hicho ulioanza Aprili, 2017.
“Vunjeni makundi chaguzi zimekiwasha tujikite kwenye kukiimarisha chama. CCM haitamvumilia mtu mwenye kuendeleza makundi,” amesema Magufuli.

MAGUFULI AKIHUTUBIA

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search