Monday, 18 December 2017

MAGUFULI AMSHUKURU KIKWETE

Rais Magufuli Amshukuru Kikwete
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutoangalia rushwa wala urafiki pindi alipomchagua kugombea urais na kutaka wanachama wake kuchagua wajumbe wa Halmashauri Kuu wenye mapenzi ya dhati na chama.


Dkt. Magufuli ameonya hayo wakati  akifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo ambapo  amesema chama hicho kimedhamiria kupambana na rushwa na kwamba kama Rais Mstaafu Jakaya Kikwete angeangalia hayo basi yeye asingepata nafasi alonayo

“Msichague watu kwa urafiki au kwa sababu ya rushwa, binafsi napenda nimshukuru mzee Kikwete (Jakaya) yeye hakuangalia rushwa nadhani angefanya hivyo huenda mimi nisingepita,” amesema.

Aidha Dkt. Magufuli amewataka wanachama wa chama chake kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa chaguzi wa ndani wa chama hicho.

“Vunjeni makundi chaguzi zimekiwasha tujikite kwenye kukiimarisha chama. CCM haitamvumilia mtu mwenye kuendeleza makundi,” amesema

Pamoja na hayo Dkt. Magufuli ameweka wazi hatosita kutengua matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu iwapo itabainika rushwa imetumika.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search