Monday, 18 December 2017

MAJONZI NA VILIO KUAGWA KWA MIILI YA ASKARI 14 WA JWTZ WALIOUAWA, DRC -(VIDEO)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiaga miili ya askari hao.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji kuaga miili ya askari 14 waliouawa na waasi wa ADF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambapo shughuli ya kuaga miili ya askari hao imefanyika leo Alhamisi, Desemba 14, 2017 katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga jijini Dar es Salaam.

Kaasim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.
Viongozi wengine waliohudhuria katika kuaga miili hiyo ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, wakuu komandi za anga, maji, nchi kavu na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), viongozi wa Umoja wa Mataifa, na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, askari na wananchi.


Zitto Kabwe akiaga miili ya marehemu hao.
Akizungumza wakati wa shughuli ya kuaga miili hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema;
“Kidiplomasia tunatumia nafasi hii kwenda kusaidia mataifa ya wenzetu ndio maana tumeshiriki katika vita za ukombozi kwenye nchi kadhaa za Kusini mwa Afrika, pia shughuli za kulinda amani katika nchi mbalimbali.

Majaliwa akisalimiana na CDF Venance Mabeyo.
“Hivi sasa jeshi letu linaendelea na shughuli hizo nchini Lebanon, Dafur na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na katika nchi zote hizo maaskari wetu wanasifiwa kwa uvumilivu, uhodari wa kazi, na nidhamu ya hali ya juu,” alisema Majaliwa.
Baada kukamilika shughuli ya kuaga miili hiyo itasafirishwa kwao mazishi.

VIDEO YA TUKIO ZIMA LA KUAGA

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search