Saturday, 23 December 2017

Mchepuko wa Dai Wakinukisha Madale Ambwagia Zari Mtoto

Mchepuko wa Dai Akinukisha  Ambwagia Zari Mtoto Madale
 Mambo ni moto! Mrembo Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amebwagiwa mtoto getini kwake na mwanamke anayedai kuzaa na baba watoto wake.

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo makini, Zari alikutana na kimbwanga hicho hivi karibuni, wakati Zari alipotinga nchini katika harusi ya shemeji yake ambapo mwanamke huyo, aliyedai ni raia wa Kenya aliona afike nyumbani kwa mchumba wa Zari, Madale jijini Dar ili kuomba msaada kwa mwanamke mwenzake. “Alishahangaika kwa upande wa mzazi mwenzake Zari akaona hapati msaada wowote sasa alivyotonywa kuwa Zari yupo mjini akaona atumie mwanya huo kwani huenda akamsaidia kama mwanamke mwenzake.

“Kiukweli Zari amekuwa akikutana na changamoto kubwa sana kwenye mapenzi yake kwa maana kwamba hivi karibuni tu baba watoto wake wawili, amezaa na Hamisa hata kabla halijaisha vizuri amejitokeza na akiwa na kichanga akisema amezaa na msanii huyo. “Mkenya huyo alilala getini kwa Zari ambapo sungusungu walimkuta na kumchukua kisha kumpeleka kwa mwenyekiti maana alikuwa akitia huruma kwani mtoto alikuwa akiumwa na mbu mno,”kilisema chanzo.

Baada ya gazeti hili kupata habari hiyo, lilifunga safari mpaka Madale, Dar kwenye serikali ya mtaa anaoishi mwanamuziki huyo, ambapo ilikutana na mjumbe wa mtaa wa Mivumoni aliyejitambulisha kwa jina la Christina Chilumba ambaye alikiri kuwepo kwa habari hizo. “Ni kweli huyo mwanamke alikuja na kulala na mtoto wake pale getini kwa msanii huyo baadaye alipelekwa ustawi wa jamii lakini zaidi mtafuteni mwenyekiti ambaye kwa sasa yuko kikaoni yeye atawaeleza kwa undani zaidi,” alisema mjumbe huyo.

mwanamuziki huyo, ambapo ilikutana na mjumbe wa mtaa wa Mivumoni aliyejitambulisha kwa jina la Christina Chilumba ambaye alikiri kuwepo kwa habari hizo. “Ni kweli huyo mwanamke alikuja na kulala na mtoto wake pale getini kwa msanii huyo baadaye alipelekwa ustawi wa jamii lakini zaidi mtafuteni mwenyekiti ambaye kwa sasa yuko kikaoni yeye atawaeleza kwa undani zaidi,” alisema mjumbe huyo.

MWENYEKITI ATHIBITISHA

Risasi Mchanganyiko lilimtafuta mwenyekiti anayejulikana kwa jina la Deo Kamugisha ambaye alieleza kwa undani tukio hilo na jinsi alivyohangaika lakini msanii huyo aliitwa ustawi wa jamii lakini mpaka sasa hajaenda hivyo utaratibu unafanyika ili apandishwe mahakamani. “Kundi la sungusungu wanaolinda mtaa wetu usiku, walikuwa wanapita maeneo ya nyumbani kwa msanii huyo wa Bongo Fleva na kumkuta mwanamke akiwa na mtoto wake mchanga akiwa amelala getini na walipomhoji ilibidi waniamshe ili nije kumsikiliza.

“Nilitoka usiku huo wa saa nane na tukamhoji ambapo mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Pansheni Salama alieleza kuwa ametokea Kenya na amefika Dar kwa ajili ya kumletea mtoto msanii huyo kwani amezaa naye. “Alieleza kwamba alianzia Ustawi wa Jamii, Magomeni akapewa barua ya wito ndiyo alikuwa akimsubiri hapo getini akitoka tu ampe ikiwa ni baada ya kutoka ofisini kwa msanii huyo Sinza lakini hakufanikiwa kumuona.

“Bahati nzuri wakati tunaendelea kumhoji, msanii huyo naye alitokea na kutoa shilingi elfu sitini na tano ambapo elfu kumi na tano ilitumika kama nauli ya Bajaj ya kumpeleka Sinza ambako msanii huyo alisema apelekwe baada ya kumpigia meneja, elfu hamsini akasema zimsaidie,” alisema mwenyekiti huyo. Aliendelea kusema kwamba msanii huyo aliitwa ustawi wa jamii mara tatu lakini hakufika hivyo kesi hiyo inatarajiwa kufikishwa mahakamani. “Jamani huyu dada siyo chizi kama maana mama wa msanii anavyosema bali ana akili timamu kabisa na ni binti aliyesoma maana ana dokomenti zote muhimu zinazomuhusu yeye na mtoto wake.

“Kiukweli tunapata usumbufu mkubwa sana na msanii huyo kwani tunatumia hela zetu kuwarudisha makwao watu wanaomfuata bila mafanikio kwani amekuwa hasikilizi watu, namshauri tu angewasikiliza watu au kuwa na sehemu yao maalum ili kutupunguzia mzigo tunaokumbana nao,” alisema mwenyekiti.

Gazeti hili lilizungumza na mwanamke huyo raia wa Kenya ambapo alirejea stori nzima iliyosimuliwa na mwenyekiti lakini zaidi akadai atapambana hadi pale mwanaye itakapopatikana. Hata hivyo, chanzo kingine cha kuaminika kilipenyeza habari kuwa, dada huyo inabidi achunguzwe zaidi kwani alishawahi kudai pia mtoto huyo ni wa msanii wa Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ miezi michache iliyopita. Alipoulizwa kuhusu hilo, alikiri kuwa ni yeye lakini alifanya hivyo kimakosa kwa kushindwa kutambua baba halisi wa mtoto lakini kwa sasa amejiridhisha kuwa mtoto huyo amezaa na mzazi mwenzake Zari

 Chanzo: Global Publisher

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search