Thursday, 14 December 2017

Miili ya Askari wa JWTZ Waliouwawa Kongo Kuagwa Kesho

Miili ya Askari wa JWTZ Waliouwawa Kongo Kuagwa Kesho


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linategemea kuaga Miili ya Mashujaa wetu waliouwawa wakiwa katika Jukumu la Ulinzi wa Amani nchini DRC hivi karibuni.

Marehemu wataagwa rasmi kesho Desemba 14, 2017 kuanzia saa 2 asubuhi  katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Upanga jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe. Dkt Hussein Mwinyi ataongoza kuaga Marehemu hao. Aidha, wananchi wote wanakaribishwa katika kuaga Miili ya Mashujaa wetu

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search