Wednesday, 13 December 2017

MWALIMU MKUU AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUBAKA WANAFUNZI 9

MWALIMU wa Shule ya msingi, Itiryo tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara, Samwel Mariba Daniel (29) amefikishwa katika mahakama ya wilaya Tarime akituhumiwa kuwabaka wanafunzi wake tisa wenye umri wa chini ya miaka 10 kwa nyakati tofauti kuanzia mwezi Agosti na Novemba mwaka huu.

Akisomewa mashitaka hayo ya ubakaji katika kesi ya jinai namba 682/2017 mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Amon Kahimba, Mwendesha Mashitaka wa Polisi Inspekta Saumu Ngoma alidai kuwa mtuhumiwa Mariba alitenda makosa hayo kati ya ubakaji kwa nyakati tofauti kwa wanafunzi wake wa darasa la kwanza na la pili kati ya Agosti na Novemba mwaka huu 2017.

Mwendesha mashitaka alidai kuwa, wanafunzi hao wa kike chini ya miaka 10 ambao majina yamehifadhiwa walibakwa na mwalimu huyo kwa nyakati tofauti wakati wakiwa maeneo ya shule hiyo kwenye nyumba za walimu. 

Alidai mwalimu alikuwa akiwatuma na kisha wanapokuwa ndani ya nyumba alikuwa akitenda kosa hilo.
Chanzo- Habarileo

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search