Tuesday, 26 December 2017

MWANAMKE AMUUA MUMEWE KWA KUMCHOMA MOTO NDANI YA NYUMBA


Jeshi la polisi mkoa wa Mtawara  linamsaka mwanamke anayefahamika kwa jina la Zuhura Ismail (29) mkazi wa halmashauri ya Nanyamba kwa kosa la kumuua mume wake
kwa kumfungia ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi kisha kuichoma kwa petroli kutokana na wivu wa kimapenzi.

 Inaelezwa kuwa Zuhura alifika kwa mume wake huyo ambaye walikuwa wametengana kwa muda na kuhisi kuwa ndani ya nyumba hiyo mumewe alikuwa amelala na mwanamke mwingine hivyo kuamua kuichoma moto nyumba hiyo na kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Lucas Mkondya amesema tukio hilo limetokea juzi ambapo mwanamke huyo alikuwa ametengana na mumewe na alihisi anaishi na mwanamke mwingine kweye nyumba hiyo na kutokana na wivu aliichoma moto.

"Kwa wivu wake wa mapenzi inasemekana Zuhura alidhani huyo mwanamme alikuwa na mwanamke mwingine ndani ya nyumba kwa hiyo alienda usiku akachukua petroli akamchoma kwenye hiyo nyumba,matokeo yake huyo mwanaume aliungua sana na akawa amepoteza maisha",aliongeza Kamanda Mkondya.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search