Saturday, 23 December 2017

Nabii Amnunulia Zawadi ya Gali la Milioni 926 Mwanaye wa Miaka Minne

Nabii Amnunulia  Zawadi ya Gali la Milioni 926 Mwanaye wa Miaka Minne
NABII wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering, Shepherd Bushiri, amemfanyia sapraizi mwanayae wa kike, Israella Bushiri mwenye umri wa miaka 4, baada ya kumnunulia gari aina ya Maserati Levante lenye thamani ya Sh milioni 926, kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.

Gari alilonunuliwa na baba yake.

Bushiri alitumia ukurasa wake wa Facebook ku-share picha na kuandika maneno ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya pekee aliyomjalia kumpata binti yake huyo.

Nabii huyo ambaye mara nyingi anafanya kazi zake za uinjilishaji nchini Afrika Kusini aliandika: “Ninaona baraka zako Mungu kwa zawadi hii ya pekee uliyonipa katika maisha yangu. Ninasherehekea kuzaliwa kwa Mungu wangu na mwokozi wangu Yesu Kristo, na kuzaliwa kwa binti yangu wa kwanza, Israella Bushiri.

“Ninaona ni kama jana tu wakati mtoto huyu alipozaliwa na kumbeba mikononi mwangu, lakini leo naweza kumweka mabegani mwangu na akatulia mwenyewe pasipo kushikiliwa, nitamsaidia kwa kila ninaloweza akue na kufikia malengo flani,” aliandika Bushiri

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search