Monday, 4 December 2017

NASARI AVAMIWA NA WATU WASIOJULIKANA RISASI ZARINDIMA

MBUNGE WA CHADEMA JOSHUA NASSARI AVAMIWA NA WATU WASIOJULIKANA...RISASI ZARINDIMA

Seebait.com 2017SeeBait

Watu wenye silaha wamevamia nyumbani kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha Mhe.Joshua Nassari maeneo ya USA River, usiku wa kuamkia leo na kufyatua risasi kadhaa ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nyumbani hapo. 

Nassari na mkewe walifanikiwa kutoroka, kisha kuripoti tukio hilo Polisi. Kamanda wa Polisi Arumeru, amesema wanafanya uchunguzi kubaini watu hao.

Haya ndiyo maneno ya Joshua Nassari kupitia ukurasa wake wa Twitter

Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search