Wednesday, 6 December 2017

POLISI WAMWACHIA KWA DHAMANA ALIYESAMBAZA PICHA ZA JENGO LENYE NYUFA

Mbunge wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Kumbusho Dawson ameachiwa baada ya kuhojiwa na polisi wa kitengo cha makosa ya mtandao.


Kumbusho alipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi leo Jumanne Desemba 5,2017 akitokea Oysterbay alikokwenda kuripoti asubuhi baada ya kuachiwa kwa dhamana jana usiku.


Wakili Alex Masaba anayewakilisha Kumbusho amesema polisi wamemuachia baada ya mahojiano na wanaendelea na upelelezi hivyo wakimuhitaji watamwita.


Masaba amesema mteja wake amekamatwa kwa kosa la kusambaza picha zinazoonyesha nyufa kwenye jengo la mabweni ya chuo hicho. Hata hivyo, amesema anaamini kilichofanyika si jinai.


"Kosa la kusambaza picha zilizopigwa si jinai hata polisi nimewaeleza kwa kitendo kilichofanyika inabidi apongezwe," amesema Masaba.Chanzo- Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search