Monday, 11 December 2017

RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 8157, BABU SEYA NA MWANAE NAO WAPTIWA MSAMAHA NA RAIS


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli leo ametoa msamaha kwa wafungwa 8157 ambapo wafungwa 1828 wataachiwa huru leo na 6329 watapunguziwa muda wao wa kifungo, Pia ametoa msamaha kwa wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa na kuziagiza idara husika kuwatoa leo au kesho.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa Tanzania tuna wafungwa 39,000 mpaka jana, kati ya hao 37,000 ni wanaume na 2,000 ni wanawake huku Wanaosubiri kunyongwa wakiwa ni 522, wanaume 503, wanawake 19 tu.

Wakati huo huo Rais Dkt. Magufuli ametoa msamaha kwa Familia ya Nguza Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha), ambao walihukumiwa kifungo cha maisha miaka kadhaa iliyopita, hivyo kuanzia leo familia hiyo iko huru.


Rais Dkt. Magufuli ametoa misamaha hiyo leo katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara, yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search